Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Adv. Julius Mtatiro amewaagiza Watendaji wa Kata kushirikiana na uongozi wa shule kufanya mikutano ya mara kwa mara ya kuwahamasisha wazazi kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata chakula wawapo Shuleni.
Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 ngazi ya wilaya ambacho kimefanyika Mei 22, 2024 katika ukumbi wa Karijuna uliopo Manispaa ya Shinyanga .
Akizungumza katika kikao hicho Adv. Mtatiro amesema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya lishe bora na uelewa wa wanafunzi.
“.......tunahitaji kuwa na kampeni kubwa sana katika hili eneo kwa hiyo niwaombe kwenye shudhuli zenu za uhamasishaji, kwenye vikao na mikutano ya hadhara hii iwe miongoni mwa ajenda yenu kubwa” alisisitiza Adv. Mtatiro
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba amewataka watendaji wa Kata kuendelea kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata lishe bora wawapo shuleni.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lishe, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Shadrack Daimon amesema Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imefanikiwa kuwapatia mafunzo ya upimaji hali ya lishe na unasihi wa mada za lishe kwa Wahudumu wa Afya 106 kutoka ngazi ya jamii na Wataalam 22 kutoka vituo vya Afya na Zahanati . Pia, mafunzo ya tathimini ya hali ya lishe na unasihi wa lishe yametolewa kwa makundi maalum kama Wajawazito, watoto chini ya miaka 5 na wanawake wenye umri wa kuzaa.
wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro akizungumza wakati wa kikao
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinynga Ndg. Kisena Mabuba
akizungumza wakati wa kikao
Afisa Lishe wa Halmashauri Ndg. Shadrack Daimon akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Januari - Machi
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.