Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji Ndg. Samson Lutonja kwa kushirikiana na Kitengo Cha Sheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wametoa elimu ya Umuhimu wa ulipaji wa ushuru wa huduma kwa wafanyabiashara wa Kata ya Salawe.
Ndg Lutonja amesema ushuru wa huduma unatozwa na kukusanywa na Halmashauri kwa mfanyabiashara kutokana na huduma anazotoa kwa kutumia miundombinu ya Umma inayomwezesha kufanya Biashara katika eneo husika kama maji na barabara.
Akifafanua zaidi Wakili wa Serikali kutoka Halmashauri Wakili Aman Mkwama amesema ushuru wa huduma unasimamiwa na Sheria inayoratibu fedha ya Serikali za Mitaa na Sheria ndogo ndogo za Halmashauri.
Aidha, Wakili Mkwama amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria mfanyabiashara yeyote atakayekiuka sheria ya ulipaji wa ushuru wa huduma atakuwa ametenda kosa linaloweza kupelekea kutozwa faini isiyopungua 200,000/= na isiyozidi 1,000,000/=
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.