Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wametakiwa
kujenga mahusiano mazuri kati yao na walimu na jamii ili kuongeza ufaulu na kuondoa utoro kwa wanafunzi.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Mwl. Andrew Mitumba wakati wa
kikao cha tathimini ya matokeo ya Moko wilaya na mkoa kilichofanyika Julai 02, 2024 katika ukumbi wa mikutano
wa halmashauri.
Wakijadili mipango mikakati ya kuinua ufaulu na kuondoa utoro kwa wanafunzi, watendaji hao wamekubaliana kuinua
ufaulu wa wanafunzi kufikia 85% kwa mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na la nne 2024.
Mikakati mingine iliyowekwa ni pamoja na kubaini mada ngumu zinazo washinda wanafunzi na kuongeza nguvu ya
ziada katika ufundishaji, kuhakikisha shule zote zinatoa chakula kwa wanafunzi na kutoa mazoezi mengi kwa wanafunzi
ili kuwajengea uzoefu na kujiamini.
Pamoja na maelekezo aliyoyatoa, Mwl. Mitumba amewapongeza walimu kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya
hasa matokeo mazuri ya moko mkoa ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeshika nafasi ya kwanza kimkoa
kwa kupata 78.89.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.