Watendaji wa Kata Wilaya ya Shinyanga wahimizwa kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiongoza kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa robo ya Kwanza Julai –Septemba kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Akizungumza katika kikao hicho Samizi amewataka Maafisa Watendaji wa Kata kufanyia kazi makubaliano ya kikao. Pia kutumia vikao na mikutano katika Kata zao kwa kutoa Elimu ya lishe ikiwa ni pamoja na kuwaalika Maafisa Lishe katika vikao hivyo .
Mhe. Mkuu wa Wilaya amewahimiza Watendaji wa Kata zote 26 kuendelea kusimamia na utekelezaji wa afua za lishe katika Kata zao kwa kuzingatia vigezo vya Taifa na kuendelea kutoa Elimu ya umuhimu wa lishe bora pamoja na madhara ya lishe duni.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia Shule zote zinatoa chakula cha mchana kwa Wanafunzi.
Mhe Johari Samizi alihitimisha kikao hicho kwa kuwataka Maafisa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia Usafi wa Mazingira katika maeneo yao pamoja na kutoa tahadhari ya mvua ya el nino kwa wananchi. Pia kuendelea kuhamasisha Wazazi kwenda kuandikisha Watoto Elimu ya Awali na Msingi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.