Kikao hicho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. David Rwazo.
Mhe. Diwani wa Kata ya Solwa Awadhi M. Aboud ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya Kata amehudhulia, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri, Wataalamu na Viongozi wote ngazi ya Kata.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Rwazo ametumia fursa hio kuwahimiza Viongozi katika ngazi ya Kata kuongeza usimamizi na juhudi za utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kuhakikisha Shule zote zilizopop kwenye Kata hio zinatoa Chakula kwa Wanafunzi.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi amewataka Viongozi hao kuendelea kutoa Elimu ya umuhimu wa Lishe bora pamoja na madhara ya Lishe duni.
Kwa upande wake Mhe. Diwani wa Kata ya Solwa, amepongeza utaratibu wa Wataalamu wa Halmashauri kufanya Kikao Kazi na Kamati ya maendeleo ya Kata. Pia amemshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo Kata ya Solwa na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa ujumla.
Mhe. Awadhi Aboud ameongeza kwa kuomba Serikali iendelee kuunga mkono juhudi za Wananchi katika Miradi ya maendeleo.
Baada ya Wikao wajumbe waliweza kutembelea baadhi ya Miradi ya maendeleo inayotekelezwa Kata ya Solwa. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Maabara na Vyoo Shule ya Sekondari Solwa “B”, Stendi ya Mabasi ya Solwa na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Manheigana.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.