Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa Ndg. Ally Salum Hapi (MNEC) amesema moja ya malengo makubwa ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ni kuboresha huduma ya maji nchini. Dhamira hiyo ya Rais inatekelezwa kwa vitendo baada ya Mhe. Rais kutoa maelekezo kwa watendaji wa Serikali kuhakikisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani inatekezwa Tanzania nzima.
Hayo ameyasema leo Agosti 03, 2024 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji Ng'wampandangabule, Sumbigu, Jimondoli na Zumve (awamu ya kwanza ) wenye thamani ya sh. Bilioni 2.4 unaotekelezwa na RUWASA. Mradi huu utahusisha ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 100,000 na unatarajiwa kukamilika Februari 2025
" Mradi huu maji unaotekelezwa hapa ni sehemu ya Serikali kutatua changamoto ya maji kwa wananchi na kutimiza Ilani ya Chama cha Mapinduzi "
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum ametoa shukurani za dhati kwa serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasaan, Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Katika Jimbo la Solwa
Ndg. Hapi yuko katika ziara ya siku moja katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo atatembelea miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.