Kamati ya Siasa Wilaya ya Shinyanga Vijijini chini ya Mwenyekiti wake Ndg Edward Ngelela leo Februari 20, 2024 imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kujiridhisha na kujionea hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyotetembelewa ni pamoja na kukagua barabara ya Mawaza na mradi wa maji Kilimawe, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Mishepu na ukarabati wa josho la Solwa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ndg.Ngelela amewaagiza watendaji kuhakikisha usimamizi wa maji unafanyika na vyanzo vya maji vinalindwa ili kuwa na uhakika wa maji muda wote.
Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya kukamilisha chumba cha ofisi ya walimu na chumba cha darasa katika shule ya Msingi ya Mishepu. Vile vile, ameiagiza Tarura kukamilisha ujenzi wa makaravati katika barabara ya Mawaza kwa wakati ili njia iweze kupitika kwa urahisi.
Wajumbe wa Kamati wakipata maelezo ya mradi wa ukarabati wa barabara
ya Mawaza kutoka kwa Kaimu Meneja wa Wilaya ya Shinyanga ,
Mhandisi Christina Msovele
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini,
Ndg Edward Ngelela (kushoto) na wajumbe wa kamati
hiyo wakikagua mradi wa maji Kilimawe
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini wakikagua
mradi wa josho la kuogeshea mifugo Solwa
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.