Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga imefanya ziara ya kutembelea miradi minne ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwalengo la kukagua nakujionea hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika Februari 22 ,2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndg. Mabala Mlolwa. Kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Mawemilu katika kijiji cha Mawemilu ambacho ni miongoni mwa vijiji sita vya kata ya Mwakitolyo.
Akitoa tarifa ya mradi huo, Mtendaji Kata, Bw. Faustine Buyunge amesema kuwa maamuzi ya uanzishaji wa mradi huo yalifanyika kupitia kamati ya maendeleo ya kata iliyoazimia uwepo wa shule ya pili ya sekondari katika kata hiyo. Mradi huo ukikamilika utasaidia watoto kutotembea umbali mrefu. Kwa sasa vimejengwa vyumba vitatu vya madarasa ambavo vimefikia hatua ya kupauliwa na vimegharimu kiasi cha Tsh.25,214,000.00.
Mradi mwingine uliotembelewa ni matengenezo ya barabara ya Mwakitolyo- Nyang’ombe katika kata ya Mwakitolyo wenye thamani ya Tsh. 66,344,000.00 ambao ulianza Februari 06,2024 na unataajiwa kukamilika Aprili 04, 2024 mwaka huu. Ukamilishaji wa mradi huu utawezesha barabara hiyo kupitika kwa urahisi .
Aidha, kamati imejionea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Awali na Msingi Songambele iliyopo katika Kata ya Salawe wenye thamani ya Tsh. 560,330,000.00. Vile vile, kamati imetembelea mradi wa maji ambao upo katika vijiji vya Nyaligongo na Nyang’ombe ulioanza Januari 31 na utamalizika April 30 mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu miradi hiyo, Ndg.Mlolwaamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga fedha ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na pia ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Mabala Mlolwa
akifungua bomba la maji wakati akikagua mradi wa maji unaotekelezwa
katika vijiji viwili vya Nyaligongo na Nyang’ombe katika halmasahuri ya
wilaya ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga wakikagua mradi
wa ukarabati wa barabara ya Mwakitolyo- Nyang’ombe katika kata ya
Mwakitolyo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
sehemu ya kipande cha Barabara kinachofanyiwa ukarabati
Mtendaji Kata ya Mwakitolyo Bw. Faustine Buyunge, akiwasilisha
taarifa ya mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Mawemilu
Mwonekano wa Shule ya awali ya Songambele
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shjnyanga wakikagua
ujenzi wa shule ya Msingi Songambele
Mwonekano wa mbele wa shule ya Msingi Songambele
Mwonekano wa Shule ya awali ya Songambele
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.