Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga
Vijijini Mhe. Edward Ngelela amewataka wasimamizi wa miradi kufanya usimamizi mzuri
wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuwezesha miradi
hiyo kukamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili ili kutimiza azma ya Serikali ya
kuwanufaisha wananchi.
Maagizo hayo ameyatoa Juni 04, 2024 wakati wa ziara ya kamati ya Siasa ya Wilaya
kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya, Jengo la
Utawala na ujenzi wa barabara.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ukamilishaji wa vyumba viwili vya
madarasa, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa mapya na matundu nane ya vyoo
katika Shule ya Sekondari Pandagichiza, ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri na
ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Iselamagazi.
Miradi mingine ni ujenzi wa mradi wa maji wa vijiji vya Mwampangabule, Sumbingu, Jimondoli
na Zumve awamu ya kwanza na matengenezo ya barabara ya Mwawaza –Iselamagazi.
Mhe. Ngelela ameipongeza halmashauri kwa usimamizi mzuri wa jengo la utawala la
halmashauri ambalo kwa sasa liko katika hatua nzuri ya ukamilishaji, ujenzi wa mradi wa maji,
madarasa na vyoo.
“tunashukuru kwa sasa tunaona kazi inaenda kuliko ilivyokuwa zamani…,walikuwa wameshakata
tamaa na wananchi waliamini majengo ya Serikali yanaenda pole pole…...”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amesema anayo imani kubwa na utendaji
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Kisena Mabuba na kwamba
mambo mengi yataenda vizuri chini ya uongozi wake. Ametoa rai kwa Mwenyekiti wa Halmashauri
na Baraza lake, Wakuu wa Divisheni na Vitengo kutoa ushirikiano kwa Bw. Mabuba.
Utaratibu wa Kamati ya Siasa kutembelea miradi ya maendeleo unalenga kujionea utekelezaji
wa miradi hiyo ili kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa
na kwa dhamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa wakipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya
madarasa , ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa na mashimo nane ya choo katika Shule ya
Msingi ya Pandagichiza
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.