Kamati ya Majanga na Maafa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yafika msibani kuifariji familia ya Ngassa Mtaluma kufuatia vifo vya Watoto watatu wa familia hiyo baada ya kuangukiwa na nyumba usiku wakiwa wamelala Aprili 26, 2024 Kijiji cha Mishepo, Kata ya Mwantini.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Miembeni B, Bw. Maasai Senema alisema tukio hilo limetokea kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kupelea nyumba kuanguka. Ndani ya nyumba hiyo walikuwa wamelala watu watano ambapo wawili wamenusurika kifo akiwemo Mama mzazi wa Marehemu hao Bi. Kashinje Nchembi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt.. Nuru Yunge akizungumza katika mazishi ya watoto hao alitoa pole kwa familia ya Mtaluma na kueleza kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa familia hiyo na kugharamia matibabu ya Bi. Kashinje Nchemmbi, Mama mzazi wa marehemu hao ambaye anaendelea na Matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Aidha, Dkt Yunge aliwataka Wananchi kujenga nyumba imara kwa ajili ya usalama hasa katika kipindi cha masika. Alihimiza Wananchi wanaoendelea kuishi maeneo amabyo yako bondeni na nyumba ambazo sio imara, kupata hifadhi katika familia zingine kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Alielekeza Viongozi na Wataalam ngazi ya kijiji na Kata kufanya ufuatiliaji kubaini na kushauri wananchi walio katika hatia ya kuangukiwa nyumba zao kuhamia maeneo salama ndani ya jamii na maeeno ya taasisi za Serikali kwa ajili ya usalama wao na mali zao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwatini Mhe. Mpemba J. Jimali alishukuru Kamati hiyo kufika msibani na kufariji wafiwa. Pia alisema kamati ya maendeleo ya Kata (WDC) watafanya utafiti wa kubaini Kaya zinazoishi kwenye nyumba ambazo hazina usalama kipindi hiki cha masika ili kudhibiti majanga na maafa kabla hayatokea.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.