Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Ngassa Mboje leo Aprili 18, 2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo robo ya tatu kwa mwaka 2023/2024 yenye thamani ya jumla ya Tsh. 511,986,829.46. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri, ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum, ujenzi wa matundu ya vyoo 26 vya wanafunzi katika Shule ya Msingi ya Isela na kutembelea kikundi cha vijana cha Usanda Kwetu.
Akizungumza wakati wa kutembelea mradi wa Jengo la Utawala la halmashauri uliopo katika kijiji cha Mwamakaranga kata ya Iselemagazi, Mhe, Mboje amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba kwa usimamizi mzuri wa ukamilishaji wa jengo la utawala ambalo limefikia hatua nzuri ya utekelezaji wa mradi huo.
“…kubwa ninaloliona ni pongezi kubwa kwako Mkurugenzi na team yako……, kwa sababu tumeona mabadiliko ya kasi na viwango, spidi tunaiona sasa baada ya wewe kuchukua hatua.
Naye Ndg. Mabuba wakati akiishukuru Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kwa kutembelea mradi huo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuridhia halmashauri kupata fedha kwa ajili ya mradi huo. Ndg Mabuba aimeitaarifu kamati hiyo kuwa kwa mwaka ujao wa fedha 2024/2025, halmashauri imeidhinishiwa kiasi cha Shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la utawala.
Kasi ya ujenzi wa jengo la utawala ni juhudi mahususi ambazo zimechukuliwa ili kuharakisha ukamilishaji wa jengo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumika mapema Mei mwaka huu.
“saa nyingine Mhe. Tunakuja hapa tunakuwa wakali kweli kweli, lengo ni kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ambayo tumejiwekea, mimi nina imani kabisa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha huu, Shinyanga DC tutakuwa nyumbani kwetu, tukiishi kwetu na sio sehemu nyingine na wananchi wetu tutawahudumia kutokea hapa, kuhamia mimi Mhe. Mwenyekiti nasubiri milango tu” alisisitiza Mabuba.
Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa sasa zipo katika jengo la muda lililopo eneo la Iselamagazi lililoanza kutumika Novemba mwaka 2019 baada ya kuhama kutoka katika Ofisi zake za Makao Makuu ya halmashauri zilizokuwa zilizokuwa Manispaa ya Shinyanga. Kuhama kulilenga halmashauri kuhamia katika eneo lake la utawala ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
Muonekano wa nje wa hatua ya ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Shinyanga, Mhe. Ngassa Mboje
(mwenye tshirt ya blue) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri kuhusu hatua za ujenzi wa jengo la utawala la
Halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Kamati wakikagua mradi wa jengo la utawala
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango na
wataalamu halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.