Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Mathew Kayanda akiwasilisha taarifa yake leo Novemba 5, 2024 wakati wa Baraza la Madiwani katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 amesema halmashauri imepokea majokofu ya kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Kituo cha Afya cha Tinde.
Mapokezi ya majokofu hayo kutatatua changamoto ya muda mrefu ambayo imekuwa inawakabili wananchi wanaopoteza wapendwa wao ambao walilazimika kusafirisha miili ya wapendwa wao umbali mrefu kwenda kuitunza kabla ya maziko.
Ndg. Kayanda amelifahamisha baraza kuwa majokofu hayo yamepokelewa kwa nyakati tofauti kutoka Bohari ya Dawa ya Kanda ya Mwanza na yana uwezo wa kuhifadhi miili 6 kwa wakati mmoja huku thamani ya jokofu moja likigharimu shilingi milioni 32 za kitanzania. Taratibu za kuyasimika zinaendelea.
Akitoa salamu za Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amelipongeza baraza kwa kuendelea kuisimamia halmshauri vizuri lakini na kuwaomba waheshimiwa madiwani kuziwasilisha ofisini kwake changamoto zao walizowasilisha katika Baraza amewaomba ili aweze kuwasaidia kuzitatua.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamaring Macha amesema Madiwani wamefanya kazi kubwa ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura hivyo waendelea kuhamasisha waliojiandikisha kujitokeza novemba 27, 2024 katika zoezi la upigaji kura.
Akihitimisha taarifa yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.