KIongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Godfrey Mnzava amezindua jengo la kutolea huduma za dharura (EMD) katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambalo liko katika kijiji cha Iselamagazi baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa mradio huo leo Agosti, 12, 2024
Akisoma taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga , Dkt. Nuru Yunge amesema ujenzi wa mradi wa jengo hilo umegharimu kiasi cha shilingi 300, 000,000 ambazo ni fedha za UVIKO zilizotolewa na Serikali Kuu.
Jengo la wagonjwa wa dharura limeamza kutumika tarehe 28/2/2024 likiwa msaada mkubwa kwa kutatua kero kwa wakazi wa halmashauri ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 40 kupata huduma katika Manispaa ya Halmashauri ya Shinyanga. Ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka wa fedha 2022/2023 na kukamilika mwaka wa fedha 2023/2024.
Wakizungumza kwa wakati tofauti, wakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wnamshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaa 2024 ni Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Taifa Endelevu
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.