• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework
Government Web Framework

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwongozo wa Tovuti za Serikali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

HOSPITALI YA WILAYA YA SHINYANGA YAKABIDHIWA GARI LA WAGONJWA

Posted on: February 16th, 2024

Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga ambalo limetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo Februari 16,2024. Gari hilo limekabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospital ya Wilaya  ya Shinyanga.


Akikabidhi gari hilo, Mhe. Ahmed, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi hasa katika sekta ya afya hususani kwa wazee, wanawake na watoto.


‘’ Leo tumepata gari hili zuri na la kisasa ili litatue changamoto ya usafiri hususani kwa akina mama wajawazito. Naomba nimshukuru sana Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye kama mama amefanya jambo hili karibia nchi nzima. Kwa miaka yake hii michache amefanya makubwa sana katika miradi mbalimbali ukiwemo huu wa afya. Mimi binafsi nimekuwa Mbunge kutoka 2005 sijawahi kupata fedha nyingi za miradi kama hizi ambazo anatoa katika awamu yake kama Rais wa nchi ya Tanzania’’


Aidha, Mhe. Ahmed, amewashukuru watumishi wote wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga kwa kujitolea kwao katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa sababu wao ni sehemu kubwa sana katika kuifanya sekta ya afya isaidie maisha ya wananchi. Vile vile, amewaomba wazidi kufanya kazi kwa juhudi maana Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo kwa ajili yao na watanzania wote.


Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga, Dkt. Tom John Mtitu, amemshukuru Mbunge huyo na kusema kuwa gari hilo litatatua changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaopata rufaa katika vituo vya afya na Hospital ya Wilaya. Pia amewaomba watumishi wenzake kutunza mali na vifaa vinavyotolewa katika kuwawezesha kutimiza majukumu yao wanapokuwa wanatoa huduma za kiafya kwa wagonjwa.


Kwa upande wao wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Bi. Agnes Masanja Dogani na Bi. Jesca Charles Salawa, wakazi wa Kata ya Iselamagazi wametoa shukrani zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea gari la kubebea wagonjwa. Hii inaonyesha anavyojali  afya za kinamama pamoja na watoto hasa kinamama wajawazito ambao hukumbwa na changamoto za kiusafiri wanapokuwa katika hali ya kujifungua.



Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum akimkabidhi ufunguo

 wa gari la kubebea wagonjwa Dereva wa hospitali ya Wilaya ya Shinyanga

 Bw. Enock Mshama Leo Februari 16,2024 wakati wa hafla ya kukabidhi 

gari hilo.


Muonekano wa gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa leo 

Februari 16,2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga.


 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga,

 Dkt. Tom John Mtitu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi

 gari la wagonjwa.


Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe

 Dr. Nuru Yunge akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa


Diwani wa Kata ya Iselamagazi, Mhe Isack Sengerema akitoa neno la

 shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa


Picha ya pamoja ya Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum

 na baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga

Picha ya Pamoja ya Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum 

na baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 09, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA ( MCHUJO) KADA YA DEREVA DARAJA LA II April 15, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA TATU April 17, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI April 19, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MITI 1000 YAPANDWA KATA YA SALAWE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU.

    December 09, 2024
  • BABA BORA, SAUTI YA UMMA NA WANAWAKE VIONGOZI WAPATIWA VITENDEA KAZI

    November 15, 2024
  • WANADIDIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI NOVEMBA 27, KUPIGA KURA

    November 15, 2024
  • MASHINE YA X-RAY MBIONI KUFIKA KITUO CHA AFYA TINDE

    November 15, 2024
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.