Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga bwana Mahira leo amemuongoza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh. Jasinta Mboneko na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Katika sherehe za kugawa hati Miliki za Kimila kwenye Vijiji vya Jomu na Kasingili
Akitowa Taarifa, Afisa Ardhi huyo Alisema katika Kipindi cha Mwaka 2020/21 Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imedhamiria kupanga na kupima Ardhi katika Vijiji vya Jomu, Nyambuli (TInde) Didia, Iselamagazi, Kasingili na Mwalukwa. ni Matarajio ya Halmashauri kuwa Upimaji huo utazalisha viwanja 1.000 na Mashamba 500 katika miji ya Tinde (Jomu na Nyambui), Didia, Iselamagazi, Kasingili na Mwalukwa,
Akieleza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Bwana Mahira Alisema. Hadi kufikia Novemba 2020, JUmla ya Hati za hakimiliki za Ardhi 89 zimeandaliwa na 29 zimechukuliwa na walengwa katika maeneo ya Salawe, Tinde na Didia. na Hakimiliki 20 zitatolewa leo tarehe 27/11/2020 kwa Wananchi wa Kijiji cha Jomu.
aidha Afisa Ardhi huyo alimueleza Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kuwa Mashamba 270 yamepimwa katika VIjiji vya Kasingili na Mwalukwa, kati ya Mashamba hayo, 172 yameandaliwa hati za Hakimiliki za kimila ambazo zitagaiwa leo tarehe 27/11/2020. maandalizi ya kukamilisha Hati zilizobkia katika vijiji vya Kasingili na Mwalukwa yanaendelea. Upimaji wa Mashamba katika Vijiji vya Kasingili na Mwalukwa unafanywa kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na shirika lisilo la Kiserikali la SHIDEPHA
Akieleza Malengo ya kutoa Hakimiliki kwa Mkuu wa Wilaya, Afisa Ardhi wa Halmashauri bwana Mahira aliyataja kuwa ni pamoja na:
Mwisho Kabisa Afisa Ardhi kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, alitowa Shukrani za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga, Viongozi na Wananchi wa Vijiji vya Jomu, Nyambui na Kasingili kwa kujitowa kwao katika kufanikisha zoezi hili.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.