Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Ngassa Mboje amewapongeza madiwani na watendaji wa hamashauri kwa utekelezaji mzuri wa afua za lishe uliopelekea halmashauri kupata kadi alama ya kijani inaashiria utekelezaji uliofikia viwango vizuri. Pongezi hizo amezitoa wakati wa kikao maalum cha madiwani cha kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Juni 2024.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, Mratibu wa Shughuli za Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Bw.Said Mankiligo, amesema kuwa Halmashauri kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali ikiwemo Word Vision, Kivulini na TCRS imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za lishe kwa kuzingatia viashiria vya mkataba wa lishe.
Bw. Mankiligo ameainisha kuwa katika kipindi cha Julai 2023 hadi Juni 2024,, halmashauri imefanya jitihada kubwa katika utekelezaji wa afua za lishe ikiwa ni pamoja na kutenga kiasi cha shilingi 93,908,580 na kutumia kiasi cha shilingi 93,805,044.5 sawa na asilimia 104.
Afua zingine zilizotekelezwa ni utoaji wa huduma ya chakula shuleni, utoaji wa vidonge vya kuongeza wingi wa damu (FEFO/ IFA) kwa wajawazito, utoaji wa matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miaka mitano, upimaji wa hali ya lishe na matibabu ya utapiamlo mkali, uendeshaji siku ya afya na lishe ( SALIKI) , utoaji wa unasihi wa lishe kwa wazazi/walezi wenye watoto kuanzia miezi 0 hadi 23 na kaguzi ya vyakula kila robo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Dkt. Kalekwa Kasanga akizungumza wakati wa kikao hicho, ametoa wito kwa madiwani kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi kula mashuleni. Amesema kuwa ulaji wa chakula mashuleni utawezesha wanafunzi kuwa na afya njema, kupata ufaulu mzuri na kupunguza utoro.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.