HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA BENKI YA NMB
Na. Afisa Habari Shinyanga DC.
Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Said Kitinga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amepokea vifaa tiba kutoka NMB vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 25, ( Viti Mwendo 5, Vitanda Mwendo 4, Magodoro 20, Vitanda vya Wagonjwa 20, Mashuka 150, Vitanda vya kujifungulia 4). Vifaa hivyo vitatumika katika vituo vitatu vya kutolea huduma za Afya ambavyo ni; Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya, Zahanati ya Lyabukande na Zahanati ya Mwabenda. Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akiongea katika makabidhiano hayo Ndg. Kitinga amesema, vifaa vitasaidia kuboresha utoaji huduma za afya. Amehimiza watumishi kutunza vifaa na kuhakisha vinatumika inavyotakiwa ili kuleta manufaa yanayotarajiwa.
Pia, ameongeza kusema kitendo cha NMB kuichagua Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kimeonesha ushirikiano kati ya Halmashauri na Benki ya NMB.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amewashuruku NMB kwa kuamua kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuwa sehemu ya upokeaji faida kwa jamii. Pia amewaomba NMB kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kusaidia juhudi za Serikali za kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Simon Berege. Ameishukuru NMB kwa mchango huo katika sekta ya afya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Aidha, Mkurugenzi Berege amesema bado kuna changamoto mbalimbali katika utoaji huduma za Afya kama idadi ndogo ya wataalam na Gari la wagonjwa, hivyo anaomba NMB na wadau wengine waendelee kuunga mkono juhudi za maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa ushirikiano na kwa kuwatambua kama Wadau wa maendeleo na kusema kila mwaka imekuwa ikitenga 1% kwa ajili ya kurudisha faida kwa jamii na wamelenga Sekta ya Afya, Elimu na Majanga mbalimbali.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.