HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KILA JUMATATU CHA WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO LEO 19.12.2022Afisa Habari Shinyanga DCBAADHI YA WAUU WA DIVISHENI NA VITENGO, WAKIFATILIA KIKAO ASUBUHI YA LEO.Akifunguwa Kikao hiko, saa 2 na Nusu Asubuhi, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu ambaye ni Katibu wa Kikao hicho,aliwataja Wakuu wa Divisheni na Vitengo wataokuwa na Mada za kujadiliwa kwenye kikao hicho kuwa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Kaimu mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mkuu wa divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na lishe, Mkuu wa divisheni ya Elimu ya Sekondari, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu na Mwisho Kabisa kuna kawaida ya kupokea Ujumbe toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.Akiwasilisha Mada kwenye kikao hiko, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu aliitarifu timu ya Menejimenti kuwa kumekuwa na hitilafu kwenye vifaa vya Tehama, na kuwa ‘Router’ imekufa na hivo, inahitaji kubadilishwa na kununuliwa nyengine. ‘Wakuu wa divisheni na Vitengo, napenda kuwajulisha kuwa tutakuwa na « Breakdown » ya Mfumo wetu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuwa kimoja kati ya kifaa chetu kimeharibika’ juhudi zinafanyika kuhakikisha kifaa kipya kinapatikana haraka iwezekanavyo’ alisema Kaimu huyo wa TEHAMA.KAIMU MKUU WA KITENGO CHA TEHAMA (Mwenye Kitambaa).
Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi aliwasilisha Taarifa ya Mafunzo juu ya uwezeshwaji kwa Maafisa 12 toka Shinyanga DC kwa muda wa siku 2 mkoani Tabora kuhusuiana na Mradi Kabambe wa Boost, unaotarajiwa kutekelezwa Wilayani Shinyanga. Alisema kuna mambo kadhaa yaapaswa kufanyika, lakini kubwa zaidi na la wazi ni jitihada kufanyika uhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule za Awali ufanyike. “Jitihada zinatakiwa sana kwani kwa sasa tuna takwimu za takribani watoto asilimia 60 wameshaandikishwa, hivo tunataraji kabla ya kuanza masomo haya Januari, uandikishaji uwe Asilimia 100 au zaidi” Alisema Mkuu huyo Bi. Bukori.
Kaimu Mkuu wa divisheni ya Miundombinu na maendeleo vijijini na mijini, aliwasilisha Taarifa kuwa Siku ya Alhamisi, tarehe 22/12/2022 kutakuwa na zoezi la kupanda Miti katika kata ya Mwalukwa, na kuwa wakuu wa Divisheni na Vitengo wote wanakaribishwa, alisema watashirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la OPE wanategemea kupanda miti katika kata hiyo.
BAADHI YA WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO, WAKIWA KWENYE KIKAO
Mkuu wa divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na lishe Aliitarifu timu ya Menejiment kuwa Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri umeshaandaliwa na utakuwa shirikishi sana. Pia aliijulisha Menejiment kuwa CHMT wote na wakuu wa Vituo (Incharges) wote wameshaanza kukutana kwa muda wa siku 5 kwa ajili ya mpango kabambe wa Afya na Bajeti.
Baada ya Majadiliano ya Kina, ikafika zamu ya Mhandisi kuwasilisha Taarifa za Miradi ya Maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Alieleza na Menejiment ilijadili kwa kina Taarifa za Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa sasa ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala, Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, Ujenzi wa Nyumba za wakuu wa Divisheni na Vitengo, Ukarabati wa Shule Kongwe Tinde na Ujenzi wa Vyumba vya madarasa 45 kweye Shule 18 Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Wajumbe walijadili changamoto na namna ya kuzitatuwa na kuridhishwa na baadhi ya shughuli namna zinavoendelea kutekelezwa.
Akiwakilisha Maagizo ya Mkurugenzi, Kaimu Murugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndugu Maduhu, alisisitiza kuwa kuwe na vikao site vya kila siku kuhaikikisha malengo ya kazi kwa siku yanawekwa na kuwa kikao cha siku kinayofuata kiwe pamoja na kuweka malengo, kinaangalia kama kuna changamoto zozote zilizopelekea kutokufikiwa kwa malengo yaliyowekwa, Alimtaka Meneja wa Mradi, Project Manager, kuwa site muda wote kuhaikisha anatowa kile alichokiita “Technical Advisory” kwa Mafundi na wataalam wengine site. Alifunga kikao Muda wa saa 4 na kuwaomba baadhi ya Wakuu wa Idara wabakie ofisini kwani ana mazungumzo nayo, Alikiahirisha kikao mpaka Jumatatu nyengine ya wiki ijayo.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.