Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Kisena Mabuba amebainisha kuwa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imepanga kujenga bweni kwa ajili ya kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalumu kupata elimu katika mazingira rafiki. Kauli hiyo ameitoa leo katika halfu ya kukabidhi msaada wa kiti mwendo kwa mwanafunzi Emmanuel Dotto mwenye mahitaji maalumwa anayesoma shule ya Msingi ya Iselemaganzi kilichotolewa na shirika la Tanzania Cheshire Foundation.
Bw. Mabuba ametoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalum kutowaficha watoto majumbani na kushindwa kuwapeleka shule hali inayopelekea watoto hao kukosa haki zao za msingi. “...Watoto wenye mahitaji maalumu sio kwamba hawawezi,wanaweza wakipewa nafasi, sisi tunasaidia ili kuwawezesha kufikia malengo yao....”
Aidha, amelishukurushirikala Tanzania Cheshire Foundationnawalimu wa shule ya msingi Iselemaganzi kwa kuwezesha upatikanaji wa msaaada wa kiti mwendo na amewataka walimu hao kufanya kazi kwa moyo wa kujitoa maana kuna dhawabu katika kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum.Walimu hao wameagizwa pia kuhakikisha kuwa wanayajua mahitaji na changamoto za wanafunzi kwa ujumla na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Iselemaganzi Mwalimu Elias Litubijawakati akitoa taarifa ya shule, ameeleza kuwa shule hiyo inaratibu zoezi la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalum na kushirikiana na wazazi ili kuhakikisha kuwa watoto hao wanapatiwa elimu.
Awali akiwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 katika Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 07 Februari, 2024, Afisa Mipango wa Halmashauri aliainisha kuwa , halmashauri imetenga mapendekezoyabajetiyakiasi cha Tsh. 128,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum.
Shule ya Msingi Iselemaganzi ina kituo cha ubainishaji na Upimaji wa Watoto Wenye Changamoto za Ujifunzaji na inatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Habari Picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Kisena Mabuba
akikabidhi msaada wa kiti mwendo kwa mwanafunzi Emmanuel Dotto wa
Shule ya Msingi Iselemaganzi kilichotolewa na shirika la Tanzania Cheshire
Foundation
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Iselemaganzi Mwalimu Elias Litubija akitoa
taarifa ya shule wakati wa hafla ya kukabidhi kiti mwendo
Baadhi ya Walimu na wazazi wakishuhudia wakati wa hafla ya kukabidhi
kiti mwendo
Baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiendelea na masomo
katika Shule ya Msingi ya Iselemaganzi.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Kamati ya Shule wakati wa hafla ya
kukabidhi kiti mwendo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.