Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba ameishukuru na kuipongeza Benki ya CRBB tawi la Tinde kwa moyo uzalendo ambao wameuonyesha kupitia ufadhili wa vifaa vya michezo. Kauli hiyo ameitoa wakati wa mapokezi jezi 16 za Mpira wa Miguu na jezi 10 kwa ajili ya Mpira wa Pete kutoka benki ya hiyo yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri Mei 02, 2024. Jezi za mpira zimetolewa ili kuwezesha Mashindano ya Michezo ya UMISETA ambayo yatahusisha michezo mbalimbali ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
“... ninawahakikishia kwamba jezi hizi zitakuwa kichocheo cha kuhamasisha na kuimarisha michezo shule za sekondari na kuibuka vipaji kwa wanafunzi wetu”.
Kwa upande wake Meneja na Tawi la Tinde Bi. Agness Mnyippembe aliushukuru uongozi wa halmashauri kwa kuishirikisha benki yao katika kufanikisha jitihada za kuimarisha michezo mashuleni ikiwa ni kielelezo kuwa Benki ya CRDB ni sehemu ya jamii.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.