Akiwasilisha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 uliofanyika Mei 10, 2024, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Stewart Makali alisema halmashauri imepokea taarifa ya uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu ambapo Aprili 30, 2024 jumla ya watu 11 waligundulika kuambukizwa ugonjwa huo katika Kijiji cha Nyaligogo Kata ya Mwakitolyo. Wagonjwa wawili walifaliki na Wagonjwa tisa walipatiwa matibabu na kuruhusiwa na Timu ya Wataalam inaendelea kufuatilia.
Aidha, alisema halmashauri imeshachukua hatua mbalimbali kukabiliana na ugonjwa huo.
“Halmashauli imegawa Dawa za kutibu maji kwa Kaya 462, tumetibu Visima vya Maji 16 na kutoa Elimu jinsi ya kujinga na maambukizi ya Kipindupindu katika Vitongoji vya Namba 1,2 na 3” alisema Mwl. Makali.
Kaimu Mkurugenzi amewataka Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuchukua tahadhari na kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu kwa kuzingatia mambo yafuatayo; kutumia choo kikamilifu, Kunawa mikono kwa Maji safi kabla na baada ya kufanya shughuli yoyote, usafi wa Mazingira kula chakula kikiwa cha moto na kunywa maji yanayotoka kwenye chanzo kinachoaminika na yawe yametibiwa.
Kwa upande wake Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amewapongeza wataalamu kuchukua hatua hizo mapema na kuwataka Waheshimiwa Madiwani kuwa msitari wa mbele kuelimisha jammi juu ya ugonjwa wa kipindupindu na kuhakikisha wananchi wanachukua tahadhari na kujikinga na maambukizi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga akifungua Mkutano
wa Baraza la Madiwani robo ya tatu wa kujadili na kupokea taarifa za
Kamati kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wa
Kaimu Mkurugenzi mtendaji akiwasilisha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Katika Baraza la Madiwani
Robo ya Tatu la kupokea na kujadili taarifa za Kamati.
w
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga
Wataalam wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.