Umoja wa mashirika manne ya ADD International, Light for the World, Sense International na Cheshire Foundation wanaotekeleza programu ya Elimu Jumuishi wamekutana katika warsha ya kujadili mkakati wa ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu.
Warsha hiyo imefayika katika ukumbi mdogo wa hotel ya karena iliyopo Manispaa ya Shinyanga leo Oktoba 18, 2024 lengo ikiwa ni kuongeza uelewa juu ya elimu jumuishi.
akizungumza wakati wa wasilisho la mabadiliko ya tabia katika jamii muwezeshaji Gerald Tuppa kutoka taasisi ya Sense International Tanzania amesema ili jamii iweze kubadilisha mitazamo ya kuwaficha watoto wenye ulemavu ni muhimu wapewe elimu ya mara kwa mara juu ya umuhimu wa elimu jumuishi.
Aidha muwezeshaji Tuppa ameongeza kuwa elimu jumuishi ikipewa kipaumbele katika jamii zetu itamuweka mtoto mwenye ulemavu mbali na unyanyapaa na kumfanya aweze kuzifikia fursa mbalimbali za kielimu.
programu hii ya elimu jumuishi inafanya kazi kwa ukaribu na mashirika ya watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Shinyanga Manispaa na Misungwi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.