Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dr. Nice R. Munissy leo tarehe 25/10/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amewasainisha mikataba ya Utendaji kazi ya Lishe watendaji wa kata na vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga akishuhudiwa na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pia akiwepo Afisa Lishe wa Mkoa wa shinyanga Ndugu Denis Madereke na wajumbe wa kamati ya Uongozi ya Afya ya Wilaya ya Shinyanga.
Dr. Nice, Akipokea Mkataba Kutoka kwa Mwenyekiti wa Watendaji wa Kata Shinyanga DC Mtendaji Maduhu.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Dr. Nice alianza kwa kusalimia Wajumbe na kuwashukuru kwa kuitikia wito wa Kuhudhuria Mkutano huo, kisha alifunguwa kikao hicho. Aliwasisisitiza Wajumbe wote waliohudhuria kuwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amesisistiza sana umuhimu wa Lishe kwa Watoto na kuonesha Madhara tunayoyapata kama Taifa, tunapokuwa na Watoto waliokosa Lishe kwa kipindi cha siku 1000. “ Mh. Rais ametuagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, tusimamie watoto wapate mlo kamili kwenye zile siku 1000” Alisisitiza Dr. Nice.
Dr. Nice R. Munissy Akishuhudia Watendaji wakisaini Mkataba wa Lishe mbele ya Kaimu DHRO Ms. Jane Gwaharagwe na DMO Dr. Nuru Y. Yunge.
Aliwakumbusha Watendaji wote kuwa inabidi tukaze buti, kwani Mkoa wetu umekuwa wa Tisa kitaifa na Shinyanga DC hatujafanya vizuri sana kwenye Taarifa ya Mwisho iliyotolewa Kihalmashauri.
Amesisisitiza kila Mdau kuhakikisha kuwa anajitahidi kuipaisha Shinyanga DC kwenye Masuala ya Lishe na yeyeyote atayekutana na Changamoto basi amfikishie haraka naye hatasita kuitatuwa kwani swala la lishe inabidi lipewe kipaumbele sana, Alisisitiza Dr. Nice.
Aliwahimiza wakuu wa Idara alioambatana nao Kwenye Kikao hiko, Mkuu wa Idara ya Fedha, Mkuu wa Idara ya Tehama, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mkuu wa Idara ya Mifugo, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Idara zote Mtambuka kuhakikisha Wataalam wetu wa Lishe na MIpango ya Lishe ipewe kipaumbele ili lengo liweze kufikiwa.
Katibu Dr. Yunge, Alisoma Agenda za Kikao hiko cha Kamati Tendaji yay a LIshe cha Robo ya kwanza yaani Julai hadi Septemba 2022 na Wajumbe wakaanza kikao mida ya Saa nne na Nusu Asubuhi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.