Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaShinyanga Bi. Hoja Mahiba amezindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi kujenga vyoo bora na kuvitumia , katika viwanja vya Shule ya Msingi Maskati, kata ya Imesela inayojulikana kwa jina la "Usichukulie poa, nyumba ni choo".
Akiongea na wananchi wa kata ya Imesela , Bi Mahiba amewataka wananchi kuhakikisha kila nyumba ina choo bora hadi kufikia Desemba mwaka huu.
Aidha, Bi. Mahiba amewaagiza viongozi ngazi za kata ,vijiji pamoja na jeshi la Sungusungu kuhakikisha wanalisimamia kwa kuhakikisha kila nyumba kuwa na choo bora na hatua kuchuliwa kwa wale wote ambao watakaidi agizo hilo .
"Tunahitaji taarifa kila wiki ya Maendeleo ya ujenzi wa vyoo bora kutoka katika kila kijiji". amesema Mahiba.
Kutoka upande wa kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Hoja Mahiba ,katikati Mhe. Diwani wa Kata ya Masengwa Bw. Nicodemus L. Simon pamoja na balozi wa kampeni Bw. Mrisho Mpoto siku ya uzinduzi wa Kampeni ya "Usichukulie poa , nyumba ni choo".
Awali akitoa taarifa ya hali ya vyoo katika kata ya Imesela, Mtendaji wa Kijiji cha Imesela Bw. Charles Bundu alisema "Ni asilimia 22 tu ya wakazi wa kata ya Imesela ndio wanaotumia vyoo bora".
Mtendaji wa Kijiji cha Imesela Bw. Charles Bundu akisoma taarifa ya hali ya vyoo katika kata ya Imesela
Naye Balozi wa Kampeni hiyo Bw. Mrisho Mpoto amesema, haiwezekani Mkurugenzi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji na kuzungumzia kujenga vyoo, hivvo kila mwananchi akawe balozi kwa mwingine kuhusu kuwa na vyoo bora na kuvitumia.
Aidha, Mrisho amewahamasisha wananchi kuachana na kasumba potofu ya kushenena vichakani na kuacha vinyesi kusambaa bali watumie vyoo bora.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.