DC SAMIZI AWASHUKURU WAJUMBE WA MKOMBOZI MINING GROUP KITALU NAMBA 11 MWAKITOLYO KWA KUMALIZA MGOGORO BAINA YAO, AWATAKA KUFANYA KAZI NA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO LENYE MGODI. AKAGUWA MRADI WA UJENZI WA MADARASA MATATU NA OFISI YA WALIMU UNAOJENGWA NA WACHIBAJI WA NAMBA 5 SHULE YA MSINGI MWAKITOLYO B
Na. Afisa Habari Shinyanga DC
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Johari M. Samizi, leo tarehe 03/05/2023 amekutana na Wajumbe wa Kikundi cha Mkombozi Mining Group, cha Mwakitolyo na kufanya nao Mazungumzo.. Akiwa na Mwenyeji wake, Diwani wa Kata ya Mwakitolyo, Mhe. Masalu N. Lusana, Afisa Tarafa Ramadhan Gideon, Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyto, Mwakilishi wa Mkurgenzi Mtendaji na Wajumbe wote wa Menejiment ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwenye Ofisi za Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Mhe. DC Alisisitiza suala la kufata Sheria na taratibu za Serikali kwenye kufanya shughuli zetu za kila siku.
Aliwashukuru wana kikundi kwa kutenga Muda wao kukutana naye na kuacha shughuli zao ambazo huwa ziko “Tight” sana. Kwa kweli nawashukuru sana ndugu Wajumbe, manake nyie watu wa Migodi huwa mko na shughuli nyingi za uzalishaji mali lakini bila kujali mmeona mje tuzungumze hapa, kwa wingi huu, nawashkuru sana na naona mna nia ya dhati ya kuhakikisha tuna songa mbele kuleta Maendeleo Mwakitolyo. Nawashukuru sana.
Awashukuru wana Kikundi kwa kufanya maamuzi ya kuungana (Joint Venture) na wawekezaji wakubwa kiasi ili kutatuwa Changamoto za Mitaji na Utaalam ambao nyie mlikuwa hamna. Nimefurahi zaidi kusikia kuwa mlishakubaliana na kufanya maamuzi mpaka hatuwa ya kusaini Makubaliano baina yenu na muwekezaji,hiki ni kitu kizuri na Serikali ya Wilaya ya Shinyanga inawapongeza sana kwa hatua hiyo,sasa tunachosubiri ni utekelezaji wa Makubaliano yenu na hawa Ofisi ya Tume ya Madini wako wanawaangalia kuona hamyumbishwi kwenye malengo mlojiwekea wenyewe.
Aliwahimiza Wanakikundi kuwa Serikali inasubiri kunufaika kutokana na Makubaliano waliyofikia wana kikundi hiko na Muwekezaji wao, na kusiwe na watu wa kuleta chokochoko baina yenu na muwekezaji kuhakikisha Masuala ya Uchimbaji na unufaikaji wa Biashara hii ya Uchimbaji inaharibika. “Hapo watatushika watu wa Serikali pabaya. Msikubali atokee mtu yeyote avuruge makubaliano yenu mlofikia, na aliwataka wanakikundi kuhakikisha Biashara hii inawanufaisha wana Kikundi wote bila Ubaguzi na kila kitu kifanywe kutokana na Katiba yenu inavosema” alisisitiza Mh DC Samizi.
Azitaka Ofisiza Tume ya Madini Mkoa wa Shinyanga kusimamia taratibu zote za uchimbaji na mikataba kuhakikisha kuwa Serikali inapata tozo zote zinatokanazo na machimbo haya na pia kuhakikisha wanawashauri mara kwa mara Vikundi hivi vya wachimbaji wadogo kufata taratibu sharia na kanuni za Serikali pamoja na kuhakikisha Katiba za Vikundi zinafatwa ili kuepusha Migogoro maeneo ya Kazi.
Asisitiza pia Halmashauri na Tume ya Madini mkoa wa Shinyanga kuhakikisha Changamoto na haki za Wanachama wa kikundi zizingatiwe sana na kuwasilishwa ofisi hizo pindi zinapotokea,pia alihimiza Usalama maeneo ya kazi upewe kipaumbele na ukaguzi wa Mara kwa mara ufanyike kuhakikisha watu wanafanya kazi sehemu salama.
Akikaguwa Mradi Ujenzi wa Madarasa matatu Shule ya Msingi Mwakitolyo B na Ofisi ya Walimu, Mradi unaojengwa kwa nguvu ya umoja wa Vitalu Mwakitolyo namba 5 Mh.
DC alisema haya ndio mambo tunayotaka, haya ndio manufaa ya kuwa na Madini na watu wakanufaika na Madini yao, aliwapongeza sana wana Vitalu hao na akasema huu ni mfano wa kuigwa na wawekezaji wote kusaidia maendeleo kwenye maeneo yenye Miradi. Kwa Taarifa tu, nimesikia kuwa Wachimbaji hawa wameshaagiza Ambulance,na kuwa iko njia muda wowote tutaipokea hapa Mwakitolyo,hatuwa hii imeifurahishasana Serikali. Tunawapongeza.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.