Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi tarehe 29 Novemba, 2023 ameongoza mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa 2022 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika ukumbi wa NSSF Shinyanga.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo haya ambayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa dini, watendaji wa kata, Mitaa na Vijiji Mhe. Samizi amewasihi washiriki wa mafunzo haya kusikililiza kwa makini ili kwenda kuwaeleza wanachi matokeo ya sensa na matumizi ya matokeo haya ili kwenda kupanga mipango endelevu kwa maendeleo ya wananchi wote kwa ujumla huku akiipongeza ofisi ya Taifa ya takwimu kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa sensa ya watu na makazi
"Kipekee naipongeza ofisi ya takwimu kwa utekelezaji mzuri wa zoezi la sensa ambalo zoezi hili kwa kupokea matokea haya yatakwenda kusaidia kupanga mipango endelevu kwa ajili ya maendeleo kwa ujumla" amesema Mhe. Samizi
Akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ndg. Mdoka Omary amesema mkoa wa Shinyanga una wakazi 2,241,299 ambapo halmashauri yenye watu wengi ni Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga watu 468,611 ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama 453,654 , halmashauri yenye idadi ndogo ya watu katika mkoa wa Shinyanga ni Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 214, 744.
Matokea haya ya sensa yatakwenda kusaidia katika kuweka mipango itakayotoa majibu ya changamoto mbalimbali za maendeleo zinazowakabili wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hususani , mipango inayojielekeza katika kuondoa umasikini wa kipato na usio wa kipato na hatimae kuinua kiwango cha hali ya maisha kama inavyoelekeza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.