Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ametoa rai kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi Novemba 27,2024 kuwachagua viongozi wa vijiji na vitongoji vyao.
Rai hiyo ameitoa leo Novemba 14, 2024 wakati akizungumza na wakazi wa halmashauri hiyo katika mashindano ya mbio za Baiskeli na michezo mingine yaliyofanyika kata ya Tinde katika uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Tinde A.
“Tuna zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 mwezi huu, ambapo zimebaki siku chache, kama tunavyofahamu, tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2024 wagombea watafanya kampeni za uchaguzi, kwa hiyo tujitokeze tukawasikilize wagombea na tarehe 27 tujitokeze tukapige kura.” amesema Wakili Mtatiro
Wakili Mtatiro amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchagua viongozi wa vijiji na vitongoji kwani viongozi hao wana majukumu makubwa yanayohusu masuala mbalimbali, ikiwemo ardhi na changamoto za kijamii na kwamba viongozi wanaowachagua watakuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
“Kati ya mambo ya hatari ambayo unaweza kufanya duniani ni kutokwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi wako wa vitongoji na vijiji kwa kuwa wana mamlaka juu ya masuala yako muhimu katika eneo lako na pakitokea changamoto ni wewe ndiye utakayepata tabu kwa hiyo niwaombe vijana, wazee, na akina mama, tujitokeze tarehe 27 mwezi huu wa Novemba, ambayo ni siku ya Jumatano siku ya mapumziko , twende tukapange foleni na tupige kura kuwachagua viongozi wetu wa vijiji na vitongoji.” amesisitiza Wakili Mtatiro
Mashindano ya mbio za baiskeli yameandaliwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt Kalekwa Kasanga yakiwa ni fursa ya kuwakutanisha wakazi wa kata ya Tinde kwa lengo la kuwahamasisha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 kuwachagua wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongozi na wajumbe wa serikali ya kijiji
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.