Wazazi na walezi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamejitokeza kuwaleta watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo yaliyotengwa kupata chanjo ya Surua na rubella. Zoezi hilo la chanjo limeanza leo Februari 15 na litamalizika Februari 18 , 2024.Chanjo ya Surua na Rubella inatolewa kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka mitano ikiwa ni ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuwakinga watoto magonjwa tajwa.
Muuguzi Bi. Martha Samweli ya Zahati ya Mwalukwa akitoa chanjo katika
eneo lililotengwa katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ngama, kata
Mwalukwa leo Februari 15, 2024
Muuguzi Bi. Njile Luhumbula akitoa chanjo kwa mtoto katika Zahanati ya
Itwangi
Daktari Issa Kalikula akimpaka mtoto wino kwenye kidole baada ya kupata chanjo katika Zahanati ya Kilimawe
Wazazi na watoto wao wakisubiri huduma ya chanjo katika zahanati ya Mendo
zoezi la Chanjo katika Zahanati ya Mwamala
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.