Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inaendelea kutoa Chanjo ya Homa ya Mapafu kwa Ng'ombe (CBPP).
Utoaji wa Chanjo umeeanza kwa Kata tatu (3) ambazo ni Mwalukwa, Nyamalogo na Pandakichizai na baadaye kuendelea katika maeneo ya Kata zingine zilizobaki.
Baadhi ya Mifugo Ikisubiri Kuingia Kwenye Uzio Huo Ili Kupata Chanjo Katika Viwanja hivi.
Afisa Mifugo wa Kata ya Lyabusalu Wilayani Shinyanga akiwa Miongoni mwa Kikosi Kazi Hiki Katika Kutoa Huduma Hii Muhimu kwa Wananchi.
Katika kuhakikisha Wananchi wananufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo Mifugo kama vile Ng'ombe, Wananchi hawa wameamua kujitokeza kwa wingi katika uchanjaji wa mifugo yao ili waweze kupata faida kupitia mifugo yao baada ya kuwa na uhakika wa kuishi kutokana na kupata chanjo ya homa ya mapafu (CBPP) ambayo ni kinga ya ugojwa huu unaosumbua sana mifugo hii kwa rika zote.
Kwa msisitizo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji bado inawahimiza wananchi kuitikia mwito huu zaidi hususani kwa maeneo yanayo endelea kuchanja ili kuwa na uhakika wa faida ya Mifugo kwa kutoathirika na homa hii mbaya kwa mifugo yao.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.