Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba, 2024.
Hayo yamesemwa leo wakati wa bonanza la michezo lililolafanyika Kata ya Salawe katika Viwanja vya Stendi ya Mabasi leo Oktoba 17, 2024.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Dkt. Kasanga amewaeleza wananchi kuwa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kunawapa sifa ya kumchagua kiongozi wanayemtaka katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Bonanza la michezo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa kukimbia na gunia, kuvuta Kamba na kukimbiza kuku ambapo washindi walipatiwa zawadi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Salawe Mhe. Joseph J. Buyugu amewataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwani zoezi la uandikishaji limeanza Oktoba 11, 2024 na litamalizika Oktoba 20, 2024 hivyo zimebaki siku tatu zoezi hilo lifungwe.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.