• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Shinyanga District Council
Shinyanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

BARAZA LA WAFANYAKAZI SHINYANGA DC LAPITISHA RASMI YA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KWA MWAKA 2023/24

Posted on: January 31st, 2023

Na Dhu’l-kifl H. Sungura-Shinyanga DC

Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC umekutana leo tarehe 31/01/2023 kwenye UKumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mjini Iselamagazi.


Akifunguwa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Maduhu, Edward. Aliwashukuru Wajumbe kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kikao hiko na kuonyesha kuwa wako tayari kupitia, kujadili, na kupitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya waka 2023/24 iliyowasilishwa na Ndugu Kayanda, Mathew ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu.

Mkutano huo ulitanguliwa na Agenda ya Uchaguzi wa Katibu na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi. Akisimimamia Uchaguzi huo,Afisa Kazi wa Mkoa wa Shinyanga, aliwaomba wagombea kujieleza kwa Wajumbe na kisha kuomba Kura. Baada ya upigwaji wa Kura kukamilika, Aliwaita wagombea wote na kutangaza Washindi, Bwana Oscar Lupavila ALichaguliwa kwa Kura 39 kati ya kura 55 zilizopigwa na hivo akapita kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC. Wakati Ndugu BI. Immaculata Msabila alipata kura 16 na hivo kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC.

Upatikanaji wa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi ukatowa Fursa kwa kikao Kuendelea na Wajumbe wakiogozwa na Mwenyekiti na Katibu walianza kujadili Agenda moja baada ya Nyengine.

Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walimumbusha Katibu na Mwenyekiti kuhakikisha wanafata sharia na taratibu za Serikali ambazo zinataka walau vyama kukutana mara mbili kwa mwaka kujadili Rasimu ya Bajeti na pia kukutana kujadiliana juu ya Mwenendo wa Bajeti. “ Sheria ndio inavotaka ndugu Wajumbe, hivo ni muhimu utaratibu huu wa Sheria uzingatiwe, Baraza likutane angalau mara mbili kwa mwaka”. Alisisitiza Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.

Kiongozi mwengine alihimiza pia kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi yahakikishe Taasisi zonatenga Bajeti Kuhakikisha wafanyakazi wanajiendeleza kielimu ili waweze kupanda vyeo vinavyotaka sifa za kimuundo kuwa na kiwango cha Elimu Fulani. “ Wafanyakazi wa Serikali kwenye Serikali za Mitaa wanapata tabu sana kwani kujisomea wakati mwengine hutakiwa kujigharamia na sio kusomeshwa na Serikali” hali ambayo alisema inawapa wafanyakazi wakati mgumu sana.

Mmoja wa Viongozi hao kwanza alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Baraza kwa kuandaa kikao kizuri kilichosheheni kila kitu, pia aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Jemedari Mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassan,kwa kuwapatia Walimu wa Shule za msingi na Sekondari Vishikwambi ambavyo sasa vinarahisisha utendaji wa kazi wa Walimu hao kidigitali. “ila naomba nitowe Ombi, Walimu hawa sasa wapewe mafunzo juu ya Matumizi ya Vifaa hivo n waelekezwe juu ya Makosa yanayoweza fayika kimtandao – “Cyber Crimes”. Alisisitiza kuwa ni vizuri Viongozi wote na wataalam wa Tehama wa Halmashauri kuandaa mafunzo hayo kwa walimu ili vifaa hivo vidumu na pia visiweze kuwaingiza matatizoni wafanyakazi wetu.


Mwisho kwenye kufunga Kikao hiko, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga akifunga kikao hicho, kwanza aliwaomba radhi wajumbe wote kuwa alishndwa kuwa nao tangu mapema kwani alikuwa kwenye Makabidhiano ya Ofisi ya Mh Mkuu mpya wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Samizi. “Ilikuwa tuwe wote tangu asubuhi lakini ikanibidi niende kwenye Makabidhiano ya Mkuu wetu wa Wilaya Mpya na anayeondoka, hivyo nawaomba radhi sana, ila kwa kuzingatia umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi, imebidi niombe udhuru kule name nije niungane na nyinyi kwenye kikao chetu muhimu cha Baraza la Wafanyakazi wa Shinyanga DC.Alianza 

kuwa kuwapongeza Viongpzi waliochaguliwa na kuahidi kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Atawapatia ushirikiano wote unahitajika kuhakikisha majukumu ya Baraza yanatekelezwa kikamilifu. Pia kuhusu mawasiliano na Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi,aliwaomba Viongozi hao kutosita kufika ofisini kwake au kuwasiliana muda wowote wanapokuwa wanamuhitaji. “ Ofisi yangu iko wazi muda wowote Viongozi mnaona kuna haja ya kuwasiliana na kuzungumza karibuni,tuzungumze maswala ya Wafanyakazi” Alisisitiza Dr. Nice Munissy.

Akifunga kikao hicho, Mkurugenzi huyo aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuwa Ofisi yake itaongeza juhudi kwenye kulipa stahiki za Wafanyakazi. “Najuwa kuna wakati mwengine baadhi ya Stahiki za Wafanyakazi huchelewa, lakini nawahakikishia kuwa hao wanaochelewesha bila sababu stahiki za wafanyakazi tutawashughulikia, alisisitiza Mkurugenzi huyo Kijana.

Aliwaomba wafanyakazi wawe huru kwenye kutowa waliyonayo moyoni na pia aliliahidi Baraza hilo la wafanyakazi kuwa kuanzia Mwaka wa Fedha unaokuja na wameshabajetia, Vikao vya Baraza hilo vitakuwa walau Viwili kama Taratibu na sharia za Serikali zinavotaka.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI - AJIRA ZA MUDA USIMAMIZI WA MIRADI November 04, 2022
  • TANGAZO LA KAZI - AJIRA ZA MUDA USIMAMIZI WA MIRADI November 04, 2022
  • UPANGISHAJI WA MAJENGO YA OFISI NA NYUMBA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA ZILIZOPO MANISPAA YA SHINYANGA July 02, 2020
  • TANGAZO MAPOKEZI YA FEDHA February 09, 2021
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UZINDUZI WA KAMATI YA WATU WENYE ULEMAVU

    February 28, 2023
  • MKUU WA WILAYA MPYA MHE. SAMIZI ATEMBELEA SHINYANGA DC, AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KATA NA KUHUDHURIA BARAZA LAKE LA KWANZA LA MADIWANI KUPITISHA RASIMU YA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA

    February 02, 2023
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI SHINYANGA DC LAPITISHA RASMI YA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KWA MWAKA 2023/24

    January 31, 2023
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI SHINYANGA DC LAPITISHA RASMI YA MPANGO NA BAJETI YA HALAMSHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KWA MWAKA 2023/24

    January 31, 2023
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa