Na Dhu’l-kifl H. Sungura-Shinyanga DC
Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC umekutana leo tarehe 31/01/2023 kwenye UKumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mjini Iselamagazi.
Akifunguwa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Maduhu, Edward. Aliwashukuru Wajumbe kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kikao hiko na kuonyesha kuwa wako tayari kupitia, kujadili, na kupitisha rasimi ya Mpango na Bajeti ya waka 2023/24 iliyowasilishwa na Ndugu Kayanda, Mathew ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu.
Mkutano huo ulitanguliwa na Agenda ya Uchaguzi wa Katibu na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi. Akisimimamia Uchaguzi huo,Afisa Kazi wa Mkoa wa Shinyanga, aliwaomba wagombea kujieleza kwa Wajumbe na kisha kuomba Kura. Baada ya upigwaji wa Kura kukamilika, Aliwaita wagombea wote na kutangaza Washindi, Bwana Oscar Lupavila ALichaguliwa kwa Kura 39 kati ya kura 55 zilizopigwa na hivo akapita kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC. Wakati Ndugu BI. Immaculata Msabila alipata kura 16 na hivo kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Shinyanga DC.
Upatikanaji wa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi ukatowa Fursa kwa kikao Kuendelea na Wajumbe wakiogozwa na Mwenyekiti na Katibu walianza kujadili Agenda moja baada ya Nyengine.
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walimumbusha Katibu na Mwenyekiti kuhakikisha wanafata sharia na taratibu za Serikali ambazo zinataka walau vyama kukutana mara mbili kwa mwaka kujadili Rasimu ya Bajeti na pia kukutana kujadiliana juu ya Mwenendo wa Bajeti. “ Sheria ndio inavotaka ndugu Wajumbe, hivo ni muhimu utaratibu huu wa Sheria uzingatiwe, Baraza likutane angalau mara mbili kwa mwaka”. Alisisitiza Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.
Kiongozi mwengine alihimiza pia kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi yahakikishe Taasisi zonatenga Bajeti Kuhakikisha wafanyakazi wanajiendeleza kielimu ili waweze kupanda vyeo vinavyotaka sifa za kimuundo kuwa na kiwango cha Elimu Fulani. “ Wafanyakazi wa Serikali kwenye Serikali za Mitaa wanapata tabu sana kwani kujisomea wakati mwengine hutakiwa kujigharamia na sio kusomeshwa na Serikali” hali ambayo alisema inawapa wafanyakazi wakati mgumu sana.
Mmoja wa Viongozi hao kwanza alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Baraza kwa kuandaa kikao kizuri kilichosheheni kila kitu, pia aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Jemedari Mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassan,kwa kuwapatia Walimu wa Shule za msingi na Sekondari Vishikwambi ambavyo sasa vinarahisisha utendaji wa kazi wa Walimu hao kidigitali. “ila naomba nitowe Ombi, Walimu hawa sasa wapewe mafunzo juu ya Matumizi ya Vifaa hivo n waelekezwe juu ya Makosa yanayoweza fayika kimtandao – “Cyber Crimes”. Alisisitiza kuwa ni vizuri Viongozi wote na wataalam wa Tehama wa Halmashauri kuandaa mafunzo hayo kwa walimu ili vifaa hivo vidumu na pia visiweze kuwaingiza matatizoni wafanyakazi wetu.
Mwisho kwenye kufunga Kikao hiko, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga akifunga kikao hicho, kwanza aliwaomba radhi wajumbe wote kuwa alishndwa kuwa nao tangu mapema kwani alikuwa kwenye Makabidhiano ya Ofisi ya Mh Mkuu mpya wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Samizi. “Ilikuwa tuwe wote tangu asubuhi lakini ikanibidi niende kwenye Makabidhiano ya Mkuu wetu wa Wilaya Mpya na anayeondoka, hivyo nawaomba radhi sana, ila kwa kuzingatia umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi, imebidi niombe udhuru kule name nije niungane na nyinyi kwenye kikao chetu muhimu cha Baraza la Wafanyakazi wa Shinyanga DC.
Alianza kuwa kuwapongeza Viongpzi waliochaguliwa na kuahidi kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Atawapatia ushirikiano wote unahitajika kuhakikisha majukumu ya Baraza yanatekelezwa kikamilifu. Pia kuhusu mawasiliano na Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi,aliwaomba Viongozi hao kutosita kufika ofisini kwake au kuwasiliana muda wowote wanapokuwa wanamuhitaji. “ Ofisi yangu iko wazi muda wowote Viongozi mnaona kuna haja ya kuwasiliana na kuzungumza karibuni,tuzungumze maswala ya Wafanyakazi” Alisisitiza Dr. Nice Munissy.
Akifunga kikao hicho, Mkurugenzi huyo aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuwa Ofisi yake itaongeza juhudi kwenye kulipa stahiki za Wafanyakazi. “Najuwa kuna wakati mwengine baadhi ya Stahiki za Wafanyakazi huchelewa, lakini nawahakikishia kuwa hao wanaochelewesha bila sababu stahiki za wafanyakazi tutawashughulikia, alisisitiza Mkurugenzi huyo Kijana.
Aliwaomba wafanyakazi wawe huru kwenye kutowa waliyonayo moyoni na pia aliliahidi Baraza hilo la wafanyakazi kuwa kuanzia Mwaka wa Fedha unaokuja na wameshabajetia, Vikao vya Baraza hilo vitakuwa walau Viwili kama Taratibu na sharia za Serikali zinavotaka.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.