Friday 4th, October 2024
@KATA YA ILOLA, KIJIJI CHA IHALO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anaawaalika Wananch wa Shinyanga kuwa kutakuwa na maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka wa 2020 yatakayofanyika katika ngazi ya Halmashauri kata ya Ilola Kijiji cha Ihalo.
Huduma mbali mbali zitatolewa kuanzia tarehe 23/11/2020 mpaka 27/11/2020 ambayo ni siku ya kilele cha Maadhimisho katika ngazi ya Halmashauri.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA NI PAMOJA NA:
1. Upimaji wa Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
2. Elimu hamasa juu ya Kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
3. TOHARA kinga kwa wanaume itatolewa kwenye Zahanati ya IHALO
4. Elimu juu ya Kupinga ukatili wa wanawake na watoto
5. Elimu juu ya Matumizi ya Kondomu na ugawaji
6. Utowaji wa Elimu na huduma za bima ya afya (CHF)
7. Upandaji wa Miti kijiji cha KASINGILI tarehe 27/11/2020
8. Utoaji wa hati za kimila itayofanyika tarehe 27/11/2020 katika kijiji cha Kasingili
9. Uzinduzi wa Matone ya Vitamin A tarehe 27/11/2020 - IHALO
10. Upimaji na ushauri wa Magonjwa yasiyoambukiza kama shiikizo la damu, uzito wa kupindukia ityofanyika siku ya Kilele cha Maadhimisho katika kijiji cha IHALO
11.Burudani mbali mbali itakuepo siku hiyo
"MSHIKAMANO WA KIMATAIFA, TUWAJIBIKE KWA PAMOJA"
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.