Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Kata na Vijiji wamekula kiapo cha Uaminifu na UTII katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Leo 30 Septemba 2024.
Wamekula kiapo hicho mbele ya Kamishna wa viapo, Hakimu mkaazi mahakama ya mwanzo Nindo Mhe. Oliva Robert Bisaga.
Hakimu Bisaga amewataka wasimamizi wasaidizi hao kuviishi viapo vyao kama Sheria ya kiapo inavyoelekeza.
Viapo hivi ni muendelezo wa matukio kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 27 Novemba 2024 ukiwa na kauli mbiu "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.