Pongezi hizo zimetolewa wakati wa Baraza la Madiwani la kupitia taarifa za kata za robo mwaka 2024/2025 lililofanyika leo Novemba 04, 2024 kwenye ukumbi wa ofisi kuu za halmashauri zilizopo Iselamagazi.
Akiwasilisha taarifa ya Kata ya Solwa Diwani wa kata hiyo Mhe. Awadhi M. Aboud amesema kata yake kupitia nguvu za wananchi wameweza kujenga shule ya sekondari yenye thamani ya shilling million 67 ambapo inafanya kata hiyo kuwa na shule tatu za sekondari
Naye Ndg. Fabian Kamoga kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga amewapongeza waheshimiwa madiwani pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri ya kuijenga halmashauri pia amekuwambusha kuendelea kuwasimamia wakusanyaji wa mapato kuhakikisha wanapeleka pesa hizo benki katika siku husika kama kanuni zinavyoelekeza.
Aidha , akifunga kikao Mh. Mboje ameielekeza ofisi ya mkurugenzi mtendaji kuendelea kuiona miradi ya maendeleo ilioanzishwa na wananchi ambayo imevuka zaidi ya asilimia 50 kuisaidia kwa kutenga pesa ya kumalizia ili wananchi waone thamani ya nguvu zao.
Taarifa za Kata zimewalishwa na kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.