Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ndg Nice R. Munissy, Aliongoza vyema Baraza lake la Kwanza kama Katibu wa Baraza la Madiwani. Akisoma Salamu zake kwa Baraza hilo mara tu baaada ya Sala ya kuiombea Halmashauri iliyosomwa na Mstahiki Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa S. Mboje, Ndugu Nice wakati akiwasilisha salaam, Alianza kwa Kumshukuru sana Mhe. Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwa Kumteuwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kisha Aliwaomba Madiwani wampe Ushirikiano kwenye kutekeleza Majukumu yake kama Mkurugenzi.
"Tumekuja Kusimamia Shughuli za Halmashauri na Serikali kwa ujumla, ni matumaini yangu tutabainisha Shughuli zote muhimu na kuanza kuzisimamia lakini Nasisitiza Mkazo uwe ni kwenye kukusanya Mapato na kuhakikisha Fedha ya Serikali tunayoikusanya inatumiwa vizuri" Alisisitiza Mkurugenzi huyo Kijana.
Mkurugenzi huyo pia aliwaomba sana Waheshimiwa Madiwani kuwa wakali kwenye Maeneo yao na kutowa usimamizi unaohitajika kuhakikisha Miradi ya Serikali inakamilishwa kwa wakati, viwango na ubora unaohitajika. "Serikali inatowa pesa nyingi kwa Ajili ya Miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yenu, nawakumbusha na ni wajibu wenu kuhakikisha mnakuwa Wakali kwenye hii miradi ili ilete tija inayohitjika. nitasikitika sana kusikia Mradi haukwenda vizuri kwenye Eneo la Mhe. Diwani wakati yeye na Team yake ya Kata wapo na walikuwa wakiangalia tu" Aliwataka Waheshimiwa Madiwani kuwa wakali kwenye usimamizi wa Miradi ya Serikali.
Akisitiza tena kwenye Ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya Mapato. Mkurugunzi huyo mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga alisema" Nawaomba Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wetu, kuwa wabunifu sana kwenye kuunda vyanzo vipya vya Mapato kwenye maeneo yetu, nakuhakisha tunasimamia ipasavyo vyanzo vilivyopo. " Ofisi yangu itatowa ushirikino wa Hali na Mali kuhakikisha tunalinda vyanzo vyetu vya Mapato vilivopo na kubuni vyanzo vipya vya Mapato katika Halmashauri yetu. Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassani ametuamini na nawahakikishia hatutamuangusha kwenye usimamizi wa Makusanyo ya Serikali na kuhakikisha tunatumia vyema mapato tunayoyakusanya.
kwa upande wao waheshimiwa Madiwani walieleza kero za Wananchi kwenye Baraza hilo na kuitaka Serikali ipatie Ufumbuzi haraka migogoro hiyo. wakiitaja baadh ya Migogoro waheshimiwa Madiwani walisema kuna mgogoro wa mipaka kati ya Wananchi wa Kata za Nyamalogo, Mwalukwa, Pandagichiza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ). "mgogoro huu umeanza kutishia usalama wa Raia na Mali zao. kuna baadhi ya wananchi wanakata miti yao na kutenegeneza kuni, lakini wanajeshi wanawanyang'anya kuni hizo wakidai maeneo hayo ni ya jeshi." Alisema Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Mwalukwa.
Lakini pia walieleza kero kubwa kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuwa ni Suala la uuzaji wa mazao ghalani. mheshimiwa DAS, Mheshimiwa Muwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, na Ndg. Mkurugenzi, "tunaomba hili swala la bei ya mazao hasa ya Choroko na Dengu lipatiwe ufumbuzi haraka. wananchi wakiuza kwa wafanya biashara bei inakuwa nzuri mpaka Sh. 1600 wakati mwengine lakini wakiuza kwa hawa sijui mnawaita AMCOS ambao ndio wanunuzi walioidhinishwa basi bei inashuka mpaka kufikia Sh. 800. hivi hizi ni hesabu gani?" Alisisitiza Mhe. Sengerema, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Iselamagazi.
Akijibu kero hizo, Mheshimiwa DAS wa Wilaya ya Shinyanga alisema Serikali imeanza kuzitafutia Ufumbuzi na kuahidi kuwa Kwenye Baraza lijalo watakuja na Majawabu yaliyofanyiwa tathimini ya uhakika na utatuzi wa kero hizo. "Tutashirikiana na Wataalam wetu, wahusika wote wa Mgogoro hiyo, wananchi na wakulima kuhakikisha tunapata majawabu ya Matatizo hayo yanayowakabili wananchi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.