Shirika lisilo la Serikali la Campaign for Female Education (CAMFED) limetoa mafunzo ya stadi za maisha
kwa Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule Sekondari, Walimu wa Unasihi Shuleni na Mratibu wa Mradi ngazi
ya Halmashauri,
Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku mbili Juni 11 hadi Juni 12, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri uliopo
Iselemagazi na yanayolenga kuwajengea uwezo makundi hayo ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza kwa
umahiri na kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababisha wasiendelee na masomo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Bw. Stewart Makal, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amesema Halmashauri iko tayari kushirikana na wadau hao
katika kuhakikisha ulinzi wa watoto katika jamii.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Filoteus Nombo akiwasilisha kuhusu dhana ya CAMFED amesema, shirika hilo lilianzishwa
nchini Tanzania mwaka 2006 likiwa na lengo la kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu ili kutimiza ndoto zake. Kwa sasa
CAMFED inafanya kazi na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sanyansi na Taknolojia katika mikoa 10. Mikoa hiyo
ni Shinyanga, Singida, Mwanza, Tabora, Iringa,Dodoma,Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Kwa upande wake Bw.Patrick Mwalyepelo, mwezeshaji wa mada ya elimu ya stadi ya maisha amesema program ya elimu ya stadi
ya maisha inalenga kumjengea mwanafunzi uwezo wa kutambua mahitaji yake ya kisaikolojia na kifizikia ili aweze kufanya vizuri
kimasomo na kimaisha. Elimu hiyo imelenga pia kuongeza mahudhurio na ufaulu shuleni.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.