TANGAZOLA KAZI - SHINYANGA DC.pdf
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anawatangazia watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb.Na.FA.228/613/01/066 cha tarehe 14.12.2023 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
1.0 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 3)
1.2.2 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
(ii) Katibu wa Kamati ya Kijiji.
(iii) Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelewa na Halmashauri katika Kijiji.
(iv) Mshauri wa Kamati ya Kijiji Kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji.
(v) Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji.
(vi) Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama.
(vii) Msimamizi na Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Kijiji.
(viii) Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi.
(ix) Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA
1.2 DEREVA DARAJA LA II
1.2.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV)
Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
1.2.2 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
(ii) Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
(iii) Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
(iv) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
(v) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
(vi) Kufanya usafi wa gari.
1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya mshahara ni TGS B.
MASHARTI YAJUMLA
‘’Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI - Computer Certificate - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)’’
“Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi waUmma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 21 Februari, 2024.
Xiii MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA,
S.L.P 113.
SHINYANGA.
xiv Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo; http;portal.ajira.go.tz/(Anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.