MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KUPITIA MPANGO WA KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARDHI, ANAYO FURAHA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA INAUZA VIWANJA KWA AJILI YA MATUMIZI MBALIMBALI KAMA MAKAZI, BIASHARA, MAKAZI/BIASHARA NA TAASISI.
VIWANJA VINAPATIKANA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KATIKA MJI WA ISELMAGAZI KANDOKANDO YA BARABARA KUU YA KWENDA SOLWA NA VINAZUNGUKA HOSPITALI YA WILAYA NA ENEO PANAPOJENGWA MAKAO MAKUU YA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI.
BEI ZA VIWANJA NI NAFUU SANA KAMA ZINAVOONEKANA KWENYE TANGAZO HAPA TANGAZO LA KUUZA VIWANJA.pdf
FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI IDARA YA ARDHI KWA ADA YA SH. 20,000 TU. MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 10/05/2022. ATAKAYEPATA KIWANJA ATATAKIWA KUKAMILISHA MALIPO NDANI YA SIKU 60 (MIEZI MIWILI) KUANZIA TAREHE ATAKAYOPEWA HATI YA MADAI.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0759 690 473, 0754 290 132
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Hakimiliki©2018. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa