Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anawatangazia watu wote wenye sifa ya kufanya kazi ya Usimamizi wa Miradi ya Ajira za Muda kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF). Muombaji awe na vigezo vifuatazo;..
1. Sifa za Mwombaji.
• Ajue kusoma na kuandika
• Awe na uwelewa /ujuzi unaothibitika katika fani za ufundi Sanifu (ujenzi/ukarabati wa malambo,Ujenzi na ukarabati wa barabara,visima vya asili na visima vifupi), uhifadhi/usimamizi wa Mazingira, Ardhi na misitu
• Utayari wa kusimamia viwango vya kazi zitakazofanyika kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi katika miradi ngazi ya jam ii;
• Awe na uzoefu wa kazi ya usimamizi wa shughuli za kijamii;
• Mwombaji aonyeshe/eleze kazi za mfano alizowahi kuzifanya.
• Kipaumbele kitatolewa kwa mwenyeji mwenye sifa kutoka katika kijiji husika au kijiji jirani.
• Asiwe kiongozi wa Serikali au Chama chochote.
• Awe na uelewa wa msingi wa matumizi ya teknolojia ya upashanaji habari kwa njia ya kielekroniki (Kishikwambi au Simu janja)
" 2. Uwajibikaji.
• Msimamizi wa Mradi ngazi ya Kijiji atachaguliwa na serikali ya kijiji kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya usimamizi wa mradi;
• Atakuwa anawajibika na kutoa taarifa kwa kamati ya usimamizi wa mradi.
3. Kazi na Majukumu:
• Kuwapangia walengwa kazi kwa kufuata vipimo vya kazi vilivyoidhinishwa;
• Kuchukua orodha ya mahudhurio ya watu wanaofanyakazi kwa kufuata mfumo ulioidhinishwa;
• Kuhakiki orodha ya vifaa, vitendea kazi na malighafi za ujenzi.
• Kuandaa na kutunza orodha ya kila siku kwa ajili ya walengwa wote walio kazini;
• Kuandaa na kuwasilisha taarifa za Wiki/Mwezi kwa kazi inayoendelea kufanyika kwa kufuata Programu ya utekelezaji iliyopitishwa;
• Kuandaa orodha ya walengwa wote waliofanyakazi na kuiwasilisha kwa
Mratibu wa Mpango wa Wilaya kwa ajili ya kufanya maandalizi ya malipo;
• Kushirikiana na wataalam wa kisekta kuhakikisha kazi zinafanyika kwa
. .
ufanisi na viwango vilivyowekwa vinafikiwa.
4. Eneo la Kazi;
• Eneo la kazi litakuwa katika Kijiji/Kitongoji mradi unapotekelezwa.
kwa Taarifa zaidi tafadhali pakuwa tangazo hilo hapa TANGAZO LA KAZI TASAF.pdf
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Hakimiliki©2018. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa