• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework
Government Web Framework

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwongozo wa Tovuti za Serikali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

Wakulima wilayani Shinyanga wanufaika na mradi wa viazi lishe

Posted on: May 27th, 2019

Mradi wa Viazi Lishe"Forgotten Crops Project" unatekelezwa na shirika la " International Potato Center "(CIP) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga .Mradi huu unatekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri na shirika la CIP chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID), kupitia kituo cha utafiti "Agriculture Research Institute".

Mradi wa viazi lishe unalenga kuboresha lishe ya watoto chini ya umri wa miaka 5 kupitia viazi lishe ,ambavyo tafiti zinaonesha vina wingi wa Vitamin A ambavyo ni muhimu sana kwa afya ya akili na ukuaji wa mtoto na kuwakinga na maradhi mbalimbali.Pia mradi unalenga kutengeneza fursa za ujasiliamali kwa wakulima, kupitia uzalishaji wa ziada wa viazi lishe ambavyo hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za kusindika kama  maandazi ,juisi,chapati ,kaukau(crips),tambi,michembe,na matobolwa ambapo mkulima anaweza kuongeza kipato chake kupitia ujasiliamali huo.

Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miezi (18) ambapo kwa sasa upo kwenye mwezi wa 7 wa utekelezaji wake.

Katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mradi unafanya kazi katika vijiji 15 ambavyo ni sayu ,pandagichiza,kadoto B, Ng`hama,shatimba,mwampangabule,mwamakaranga,mwabundala,iselamagazi,lyabusalu,mwasingu,mwashilugulu,sumbigu na bukene.

Afisa lishe wilaya bw.Mankiligo said akielezea umuhimu wa  viazi lishe kwa ukuaji wa afya ya mwili na akili kwa watoto.

Malengo ya mradi wa viazi lishe kwa wakulima wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni pamoja na :

  • Kuongeza uzalishaji na ulaji wa viazi lishe vyenye wingi wa Vitamin A kwa kutumia teknolojia za lishe na kilimo
  • Kuboresha upatikanaji wa elimu ya lishe na kuongeza matumizi ya viazi lishe kwa jamii

Mradi umetekeleza shughuli mbalimbali katika wilaya zikiwemo:

  • Mradi umetoa mafunzo kwa wakulima 504 (Me 189, ke 315) juu ya uzalishaji bora wa viazi lishe  katika vijiji 15.
  • Kuwezesha wakulima 10, wataalam ngazi ya vijiji 16 na wataalam ngazi ya wilaya 2 kujifunza teknolojia ya uzalishaji wa mbegu salama za viazi lishe kwa kutumia teknolojia ya vitalu wavu (Net tunnels)
  • Kuwezesha mafunzo kwa wahudumu wa afya ya msingi ngazi ya kijiji, ambapo wahudumu wa afya ya msingi wapatao 30 wamepatiwa mafunzo ya lishe bora kwa lengo la kufikisha elimu hiyo kwa akina mama wajawazito,wanyonyeshao na wenye watoto chini ya umri wa miaka 5 katika vijiji ambavyo mradi unafanya kazi.Pia mradi umewapatia nyenzo maalumu wahudumu hao kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Kupitia mradi wa viazi lishe mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwemo:

  • Uelewa umeongezeka kuhusu viazi lishe kuliko hapo awali kwamba ni zao la wote
  • Vikundi vya wakulima wanaozalisha viazi wameanza kupata faida mbalimbali kama kuboresha afya zao lakini pia kujiongezea kipato kupitia kuuza viazi hivyo na mbegu pia
  • Jamii imepata uelewa wa matumizi ya bidhaambalimbali zitokanazo na viazi lishe kama kutengeneza unga wa maandazi ,chapati,uji.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 09, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA ( MCHUJO) KADA YA DEREVA DARAJA LA II April 15, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA TATU April 17, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI April 19, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MITI 1000 YAPANDWA KATA YA SALAWE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU.

    December 09, 2024
  • BABA BORA, SAUTI YA UMMA NA WANAWAKE VIONGOZI WAPATIWA VITENDEA KAZI

    November 15, 2024
  • WANADIDIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI NOVEMBA 27, KUPIGA KURA

    November 15, 2024
  • MASHINE YA X-RAY MBIONI KUFIKA KITUO CHA AFYA TINDE

    November 15, 2024
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.